Home / Uncategorized / News & Events / MICHANGO YA PMS KWA MWAKA 2020 TOKA KANISA LA TANZANIA

MICHANGO YA PMS KWA MWAKA 2020 TOKA KANISA LA TANZANIA

Wapendwa familia ya Mungu. Kwa moyo uliojaa furaha na shukrani, Sekretarieti ya Tume ya Uinjilishaji ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (PMS) inapenda kuwashirikisha matokeo ya Michango ya Mashirika ya Kipapa toka Kanisa Katoliki Tanzania kwa Mwaka 2020.

Hali kadhalika, tunapenda kutumia fursa hii kuwashukuru sana mababa Askofu, mapadre, watawa, waamini walei, marafiki wa PMS na wote wenye mapenzi mema waliojitoa kwa dhati kabisa katika kuinjilisha pamoja na Baba Mtakatifu kwa njia ya sala na majitoleo yao. Kwa kuzingatia kuwa utume huu ni endelevu, tunazidi kuwaalika nyote muendelee kuunga mkono utume huu muhimu. Mwenyezi Mungu azidi kuwabariki kwa ukarimu wenu mlioonesha na kuwaongezea zaidi na zaidi.

Ili kuisoma taarifa hii, tafadhali bofya katika links zinazoonekana hapa chini.

Michango ya PMS na wachangiaji wote Р2020 

Michango ya PMS kwa ufupi – 2020