Home / Uncategorized / News & Events / UJENZI WA SEMINARI KUU MPYA

UJENZI WA SEMINARI KUU MPYA

Mwenyekiti wa bodi ya Seminari Kuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania inayosimamia ujenzi wa Seminari Kuu Mpya ya  Nazareti – Mwendakulima  iliyoko   Jimbo Katoliki la Kahama, Askofu Joseph Mlola wa Jimbo la Kigoma;  anawaomba waamini wote na watu wote wenye mapenzi mema kuchangia kwa hali na mali ujenzi wa seminari  kuu hiyo.

Seminari hiyo inatarajiwa kufungulia mwanzoni mwa mwezi wa kumi mwaka huu ikiwa na taaluma za Teologia na Filosofia.  Changia ujenzi wa seminari hiyo usaidie malezi ya waseminari wetu. Toa ukarimu wako kwa kutumia akaunti iliyopo benki ya CRDB, akaunti yenye Jina: “Nazareth Senior seminary, Mwendakulima Kahama” akaunti namba: 0150493723400 au kwa kutumia M- pesa yenye namba:  5582869, na Muamala utasoma  Nazareth Major Seminary Ujenzi”.

Kumbuka ni “Ni heri zaidi kutoa kuliko kupokea” (Matendo 20:35). Wasiliana na   Pd. Pius Rutechura anayesimamia ujenzi huo kwa namba hizi: 0745 100100 au 0746 500001.