Katika mwaka huu wa Jubilei kuu, watoto wa JNNK ya Mt. Benedicto, kigango cha Lupingu, Paroki ya Lupingu, Jimbo la Njombe wamefanikiwa kuiweka na kuitekeleza mikakati yao ya kusali Jumuiya Ndogongogo ya Kikristo kwa muda wa wiki sita kwa malengo kadhaa. Watoto hawa kwa muda wa wiki sita wamekuwa katika Umisionari wa kupita katika kila Jumuiya ndogondogo ili kuwahamasisha wenzao kuhusu Mwaka mtakatifu pamoja na kusali sala ya jubilee hii. Pamoja na kusali sala hii, wamekuwa wakifanya tathimini juu ya kazi zao za umisionari ili kuweza kuboresha zaidi utume wao na kuhakikisha kuwa wanapofika katika jumuiya nyingine za watoto wanakuwa wameshaandaa mambo muhimu ya kuwashirikisha.
Aidha, pamoja na sala ya jubilee wanayokuwa wakiisali kila wanapokutana, daima wamekuwa na utamaduni wa kusali sala ya rozari takatifu ili kumuomba mama Maria aliye nyota ya Uinjilishaji, aweze kusafiri nao kwenye utume wao.
Imeandaliwa na: Pd. Lucas Mgaya, Mkurugenzi wa PMS – Jimbo