Wakurugenzi (PMS).

  1. EXAVERY MAFWIMBO
  2. EDWINA MKARAWA

Viongozi wa Jimbo (POPF)

  1. M/Kiti: RUBEN NGAMBA
  2. M/M/Kiti: ANATORIA GAUDENCE
  3. Katibu: AVELINA MLELWA
  4. M/Katibu: RICHARD KAWANA
  5. Mhazini: ANDREA FINGA

Mnamo tarehe 22/02/2025 katika moja ya ziara za ndani ya Jimbo kwa wakurugenzi wa PMS Parokiani Vwawa, wamissionari wa POPF waliweka azimio la pamoja kuzuru mji wa Bagamoyo uliopo Pwani kwa malengo mawili mahususi.

  1. Kuhudhuria na kushiriki katika adhimisho la Misa na sherehe za kuanzishwa rasmi kwa Jimbo jipya la Bagamoyo na kusimikwa kwa Askofu wa kwanza wa Jimbo hilo ambaye ni mzaliwa wa Jimbo Kuu la Mbeya Mha. Stephano Lameck Msomba OSA.
  2. Kutembelea makumbusho ya kihistoria na kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo imani Katoliki ambapo Bagomoyo ndipo walipoingilia wamissionari na sasa panaitwa “lango la Imani”.

Wazo la ziara hii lilikubaliwa kwanza na Mhasham Askofu Mkuu Garvas G.M Nyaisonga  na kisha kuratibiwa vema nasi wakurugenzi tukisaidiana kwa ukaribu na viongozi wa POPF. Kila mwanachama alitakiwa kuchangia Tshs 150,000/= ili kufanikisha ziara pamoja na zawadi kwa Mha. Askofu Stephano Msomba wa jimbo jipya la Bagamoyo.

Wmisionari walikusanyika lilipo Kanisa Kuu la Jimbo na kisha kupata baraka ya safari toka kwa Mha. Askofu Mkuu Gervas J.M Nyaisonga na kisha safari ilianza tarehe 02.05.2024 mnamo saa12:00 jioni na kuwasili Bagamoyo tarehe 03.05.2025 mnamo saa 1:15 asubuhi. Wamisionari wawakilishi wapatao 8 walipumzika na kisha mida ya mchana walizuru maeneo mbalimbali ya kihistoria na kujifunza mambo yahusuyo imani na historia kwa ujumla. Jioni wamissionari walishiriki masifu ya jioni “Vespers” na kisha wakaendelea na shamra shamra mbalimbali. Kwa kuwawalikuwa katika vazi rasmi walitambuliwa kirahisi na kuhudumiwa kwa haraka jambo lililowatia moyo sana. Cha kuvutia zaidi ni pale watu walipowaita, kukaa nao na kuwauliza maswali mbalimbali juu ya utume wao wa kimissionari.

Ilipofika tarehe 4.05.2025, wamissionari walishiriki Misa ya kuanzishwa rasmi Jimbo la Bagamoyo na kushuhudia Askofu wa kwanza wa Jimbo Mha. Stephano Msomba OSA akisimikwa rasmi. Baada ya Misa na shamra shamra za sherehe, Wakurugenzi wote wawili pamoja na wamissionari tulianza safari kurudi Mbeya mnamo saa 1:30 usiku na kuwasili Mbeya tar 5.05.2025 mnamo saa 03:12 asubuhi.  Sambamba na taarifa hii napenda kuambatanisha picha mbalimbali za matukio tangu mwanzo wa ziara hadi mwisho.

HITIMISHO: Hakika ziara ilikuwa nzuri na ya kupendeza ambambo malengo yote ya wamissionari yalizingatiwa na kutimizwa vema. Kwa sasa zinafuata ziara za ndani katika Parokia zote 8 ambazo shirika hili limeishasimikwa rasmi, na kisha kutimiza mpango wa mwaka huu wa kulisimika shirika katika Parokia mbili zaidi ambazo ni Mwanjelwa na Mbeya Mjini na hivyo tutafikisha Parokia 10 zenye wamisionari wa POPF.

Asante

Umebatizwa………………………….Unatumwa!

………………………………………………

Fr. Exavery Mafwimbo

Mkurugenzi wa PMS Jimbo Kuu la Mbeya.