Jimboni Morogoro  katika mwaka mtakatifu wa 2025, watoto wanafanya hija kidekania, hija ambayo ni pamoja na kuzunguka na msalaba mtakatifu. Mnamo tarehe 31 Mei 2025 watoto wa parokia ya Mzumbe, walifanya hija yao ya kimisionari ambapo walisindikizwa na walezi miongoni mwao wakiwa watawa. hija hii inaonyesha kuzaa matunda kiroho kwani watoto wamekuwa wakizunguka na msalaba huu mtakatifu kwa uchaji mkubwa sana. pamoja na safari hii ya kimisionari, watoto waliweza kucheza michezo mbalimbali zikiwemo nyimbo zilizokuwa zinaelezea thamani na ukuu wa msalaba mtakatifu huku wakirejelea katika biblia 1Kor 1:18-25

 

 

Imetayarishwa na: Pd. Joachim Masangu, mkurugenzi PMS Jimbo