Jimbo katoliki la Sumbawanga mnamo tarehe 10-15 Juni 2025, lilifanikiwa kufanya kongamano lake la Utoto Mtakatifu katika parokia ya Kate. Kongamano hili lilikuwa na jumla ya watoto washiriki 820 na walezi 94. Aidha, dhamira ya kongamano ilikuwa ni Mahujaji wa Matumaini kwa kuzingatia kwamba mwaka huu wa jubilee ya kanisa umebeba dhamira hii.

 

Watoa mada katika Kongamano hili walikuwa 6 yaani; mapadre 2, masista 2 na wazazi 2 (me & ke) Fumbo la Ekaristi Takatifu, Pd. Nolascus Mwandambo OFMCap, Alama za Kanisa na Pd. Nolascus Mwandambo, Kanisa la Kisinodi, Pd Nolascus Mwandambo OFMCap, Biblia Takatifu Pd Urbano Mwanauta OSB, Liturjia ya Kanisa  Pd Urbano Mwanauta OSB, Utandawazi Pd Urbano Mwanauta, Miito Mitakatifu Sr Anwarite Yilahenda MMMMA, Watoto na Kazi  Sr  Anwarite Yilenda MMMA, Watoto na Sala Sr Sr Filomena Siyumbu MMMMA na mada kuhusu Maadili Mema ilitolewa na Wazazi wawili 2. Bw. Chole Silwela na Bi Maria Masombwe

 

Watoto walikaa siku 5 Parokia ya Kate na Walifanya Hija kwenda Abasia ya Roho Mtakatifu Mvimwa na Kurudi km 18 Jumla kwenda na Kurudi. Huko waliona Kazi mbalimbali za Watawa Wabenedictine, na hivyo kuchochea miito ya kazi kwa watoto, ikizingatiwa kuwa walifundishwa mada mojawapo kuhusu kufanya kazi.

 

 

 

Imetayarishwa na Pd. Nolascus Mwandambo, Mkurugenzi Jimbo