Mnamo tarehe 19- 21 mwezi Juni, kumekuwa na Kongamano la utoto mtakatifu kanda yaMwanza, kanda ambayo inaundwa na majimbo nane: (Mwanza, Shinyanga, Geita, Musoma, Bunda, Kayanga, Bukoba na Rulenge Ngara) kongamano hili lilikusanya watoto zaidi ya 5000. Kongamano hili lilikuwa la Hija ya watoto kanda ya ziwa kuenzi mwaka wa Jubilei 2025.

Aidha, kwa upande wa jimbo la Shinyanga washiriki watoto walikuwa ni 182, walezi 9 watawa 4 na Padre 1. Miongoni mwa mada zilizofundishwa ilikuwa ni kuhusu Bikira Maria alivyowatokea watoto watatu (Lucia, Francis na Yasinta) kule Fatima. Mada hii iliwasilishwa na Mhashamu baba Askofu Jovitus Mwijage wa jimbo katoliki la Bukoba ambaye ni Rais wa Mashirika ya Kipapa Taifa na Mwenyekiti wa mashirika ya kipapa katika kanda ya Mwanza.

Misa ya Ufunguzi wa Kongamano la kanda iliongozwa na mhashamu Jovitus Mwijage, Askofu wa jimbo katoliki la Bukoba. Watoto wa jimbo katoliki la Shinyanga nao kama washiriki wa kongamano hili, waliandaa   burudani ya wimbo pamoja na ngoma ya kisukuma ingawa muda haukutosha kuonyesha vitu hivyo vyote.

Watoto walifurahi sana kukutana na kundi kubwa la watoto wenzao na pia wengine. Kwa upande mwingine, kongamano lilikuwa kama fursa kwa watoto wengine kwani  ilikuwa ndio mara yao ya kwanza kufika jiji la Mwanza. Safari ya kwenda ilikuwa nzuri sana maana hapakuwa na changamoto lakini safariya kurudi kulikuwa na changamaoto kidogo maana tulikaa sana barabarani kwa sababu ya msafara wa Rais.

Misa ya kufunga kongamano iliongozwa na baba Askofu Flavian Katindi Kasala wa jimbo la Geita

Mimi kama mlezi, kwenye kongamano hili la kanda nimefurahishwa sana na mahudhurio ya watoto kwa ujumla na kwaya katika maadhimisho ya misa ambayo iliongozwa na watoto wenyewe. Aidha, namshukuru sana Mungu kwa baraka zake maana tulianza salama na kumaliza kongamano letu la kikanda salama.

 

 

 

Imeandaliwa na Pd. Francis Kamani, Mkurugenzi PMS jimbo