Mwezi Juni 2025, walezi 172 wa kanda ya kati ambayo inaunganisha majimbo matatu yaani: (Dodoma, Singida na Kondoa), waliweza kupatiwa semina yao na Katibu wa Utoto mtakatifu, Sr Anagladness Mrumah.  Aidha, semina hiyo ilikuwa na malengo matatu muhimu. Lengo la kwanza lilikuwa ni kuwasisitiza walezi mambo msingi ambayo watoto wanapaswa kufundishwa ambayo kwa hakika ndiyo yatakayowakuza kiroho, kiakili, kifikra na kisaikolojia. Lengo la pili lilikuwa ni kuwaeleza walezi njia mbalimbali ambazo wanapaswa kuzitumia wakati wa kuwasilisha mada zao kwa watoto ili kuhakikisha kuwa yale waliyonuia kuyaeleza kwa watoto yanaeleweka kwa urahisi. Lengo la tatu lilikuwa ni kuwaeleza walezi mambo ya muhimu ambayo wanapaswa kuyashikilia katika kazi yao ya malezi ili kusudi yawajenge na hivyo kuwa walezi bora, na hivyo kumudu utume wao.

Kwakweli ni jambo la kushukuru kuwa semina ilienda vyema kwani walezi wote walionyesha kupokea mafundisho vizuri kabisa, na kwa upande mwingine kushauriana wao wenyewe, kuuliza maswali mbalimbali na hata kuchangia hoja. Moja ya mambo mazuri ya kipekee yaliyoonyeshwa na walezi wa kanda hii ilikuwa ni uthabiti na utayari wa kuwalea watoto ambao walikuwa ndani ya kongamano lao kwa kipindi hicho yaani kuanzia tarehe 25 – 29 Juni, 2025.

Sambamba na semina hii, mababa maaskofu (mhashamu Askofu Edward Mapunda na Askofu Wilibrod Kibozi), katika homilia zao waliwatia moyo mkuu na kuutambua utume wa walezi hawa kuwa ni wa thamani na Baraka kwa Mungu. Hivyo waliwaomba kujisikia kuwa watu wa thamani katika kanisa kwani watoto ndio kanisa lenyewe.

 

 

 

Imetayarishwa na: Ofisi ya PMS Taifa