Katika safari hii tumejifunza mambo manne muhimu: wewe ni mmisionari, sala yako ni utume, upendo wako ni utume na ukarimu wako ni utume.
Sasa ni wakati wa kufanya ahadi.
Mpendwa mtoto, kuwa mmisionari si jambo la kufanya siku moja tu. Ni namna ya kuishi kila siku. Unaweza kuwa mmisionari nyumbani, shuleni, kanisani na unapokuwa na marafiki zako.
AHADI YANGU YA KIMISIONARI
Mimi ni mtoto wa Utoto Mtakatifu.
Nitasali.
Nitapenda.
Nitashiriki.
Nitatoa.
Nitasaidia.
Nitawaombea watoto duniani.
Nitawaombea wamisionari.
Nitakuwa na moyo wa ukarimu.
Nitamsaidia mtoto mwenzangu.
Kwa sala yangu, kwa upendo wangu, kwa ukarimu wangu na kwa matendo yangu, nitakuwa mmisionari wa Yesu.
Kumbuka ujumbe huu
MTOTO AMSAIDIE MTOTO MWENZAKE!
Kila mtoto ana nafasi katika Misioni. Mmoja anaweza kusali, mwingine kusaidia, mwingine kutoa, mwingine kufariji-lakini wote tunaweza kushiriki.
Mwaka 2026 tunasherehekea miaka 100 ya shukrani kwa Dominika ya Misioni tangu mwaka 1926. Ni nafasi nzuri ya kuendelea kukuza moyo wa sala, upendo na ukarimu kwa ajili ya Misioni.
Sala yangu
Mama Maria,
uombee watoto wote duniani.
Nisaidie kuwa mtoto mwenye moyo wa upendo na ukarimu.
Nifundishe kusali, kusaidia na kushirikisha wengine.
Nifanye kuwa mmisionari mwaminifu wa Yesu.
Amina.
Mimi ni mmisionari!
Sala yangu ni utume.
Upendo wangu ni utume.
Ukarimu wangu ni utume.
Matendo yangu ni utume.
Mmoja katika Kristo, tumeungana katika utume!

 

 

Imeandaliwa na: Ofisi ya PMS Taifa