Katika Parokia ya Ibwanzi Jimboni Mafinga Leo 10/05/2025 tumekuwa na Semina kwa watoto na Vijana wa Sekondari wapatao 87 kwa lengo la kufafanua Ujumbe wa hayati Baba Mtakatifu  (Fransisko XVI) wa Dominika ya Miito. Maudhui ya semina hii ilikuwa ni kwa ajili ya kuhimiza roho ya sala na majitoleo kwa wahusika hawa, ili kuwajengea ari na mwelekeo wa kutoa maisha yao kama Zawadi kwa Mungu kwa njia ya kuitikia Miito mitakatifu ya Upadre, Utawa na Ndoa. Semina ilifanikiwa vizuri kwani hadhira yetu ilionyesha kupokea mwito huu wa kumuomba Bwana wa mavuno awasaidie kutambua miito yao na hivyo waweze kujitambua na kutambua Mungu anawahitaji katika maisha yapi.

 

 

Imetayarishwa na : Pd. Gosbert Mlambia, Mkurugenzi wa PMS Jimbo