Tarehe 19-22 Juni tuliadhimisha Kongamano ya Kanda la Mwanza/Ziwa Victoria kwa ajili ya kuadhimisha mwaka wa Jubilei 2025 kwa ajili ya kuimarisha Imani ya Watoto wa Mashirika za Kipapa Kanda ya ziwa. Yafuatayo ni majimbo ya kanda ya mwanza: Jimbo kuu la Mwanza, Musoma, Bunda, Shyinyanga, Geita, Rulenge-Ngara, Kayanga na Jimbo la Bukoba.
Bukoba watoto 546, walezi 45, watawa 9,mapadre 2. Shinyanga watoto 181 walezi 9 watawa 4 padre 1. Musoma watoto 450 walezi 37 watawa 8. Bunda watoto 583, walezi 60,watawa 2, mapadre 1.Kayanga watoto 488walezi 26watawa 9 mapadre 1. Rulenge ngara watoto 515, walezi 25, watawa 5. Geita watoto 70 walezi 47, watawa 2, mapadre 1. Mwanza watoto 835 walezi 62 watawa 10, mapadre 2
Kutoka majimbo haya tajwa hapo juu walihudhuria na kufurahia Kongamano hilo wakisema :”heri ingeendelea hadi wiki nzima”. Waliahidi awamu ijayo wataudhuria wengi zaidi.
Waliudhuria watawa toka Mashirika mbalimbali wanaofanya utume wa kuwalea watoto kiimani na kimaadili.
Watoto walipata mada mbalimbali kutoka kwa watu mbalimbali kwamfano: Askofu wa Jimbo la Bukoba Jovitus Mwijage alifundisha mada :”Watoto waige maisha ya watakatifu. Mapadri wakurugenzi pia walitoa Mada kwa kukusisitiza watoto waendelee kujitambua Watoto walifurahia Mada zilizotolewa, michezo mbalimbali, burudani na nyimbo za utamaduni.
Misa ya ufunguzi iliadhimishwa na Askofu wa Bukoba, Jovinus Mwijage na Misa ya hitimisho iliadhimishwa na Askofu wa Jimbo la Geita Kasala, Flavian Kassala.
Michezo ya maswali na majibu kuhusu sakramenti, liturujia, historia ya kanisa
Michezo ya mpira kati ya mashabiki wa yanga 3-1 Simba na michezo mingine ilichezwa katika kongamano hilo.
Kongamano la Kanda Limetusaidia Yafuatayo :
Watoto kusafiri kugundua mazingira mapya.
Watoto kujifunza kupitia Mada, michezo, burudani.
Watoto walijifunza kuishi mbali na familia kwa kujitegemea.
Tunamshukuru Mungu kutuwezesha kuadhimisha Kongamano na kumaliza Salama.
Tunamshukuru Rais wa PMS, askofu Jovitus Mwijage wa Jimbo la Bukoba kwa kutulisha neno, Mada na kuhudhuria Kongamano. Tunamshukuru baba Mheshimiwa Mkurugenzi waTaifa PMS Padre Alfred Kwene kwa ushiriki wake. Aidha, tunawashukuru wakurugenzi wa majimbo yote ya Kanda ya kwa kushiriki wao mzuri. Shukran nyingi ziwaendee walezi na watoto kwa kuitikia na kuja katika kongamano hili.
Imeandaliwa na: Pd. Yvon, Mkurugenzi msaidizi wa PMS, Jimbo Kuu la Mwnza.



Today the studios of Radio Maria Tanzania roared with the voices of praying the Universal Holy Rosary, while they invited people from every group: elders, youth, businessmen, farmers, and other groups, with the concept of living the message of Pope Francis for Mission Sunday 2024 which says; Go and invite everyone to the banquet (Mt 22:9).