Archives for News & Events

KONGAMANO LA UTOTO MTAKATIFU JIMBONI IFAKARA, 2024

Mwaka huu kongamano la utoto mtakatifu katika jimbo la Ifakara, limefanyika katika parokia ya mtakatifu Francis Xavery Kisawasawa kuanzia tarehe 26-28 Disemba 2024. Kongamano hili lilikuwa na jumla ya washiriki watoto wapatao 591. Kauli mbiu ya kongamano hili ilikuwa ni Mtoto ni Malezi. Aidha, mada mbalimbali ziliwasilishwa na watu wafuatao: Uelewa juu ya Biblia Takatifu na Maadili Mema na Pd. Boniface Mwanja, Sakramenti za Kanisa na Ekaristi takatifu Pd. Edson Lyabonga.

Kongamano hili pia lilinogeshwa na maandamano ya kimisionari ambayo yalifanyika siku ya tarehe 28 na kupokelewa na baba Askofu Salitarus Libena, na baadaye misa takatifu ya Watoto Mashahidi.

Tunamshukuru sdana Mungu aliyeyawezesha haya yakaweza kufanyika kwa kadiri ya mpango wake.

 

 

 

 

 

Imeandaliwa na: Pd. Michael Mhina, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa, Jimbo

Read more

KONGAMANO LA UTOTO MTAKATIFU JIMBONI LINDI (26-28 DEC. 2024)

Watoto wa jimbo katoliki la Lindi wameweza kushiriki kongamano lao hapo Disemba  mwaka huu 2024, katika parokia ya Kilwa Masoko. Kongamano hili lilianza mnamo tarehe 26 – 28 Disemba (sikukuu ya watoto mashahidi). Washiriki watoto katika kongamano hili walikuwa jumla yao 410 kutoka katika kila parokia.

Katika kongamano hili watoto walifundishwa mada mbalimbali kama ifuatavyo: Jografia ya Biblia na Pd. Paul Chembe, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa Jimbo, Haki na wajibu wa mtoto na Pd. Fridolin Makwinya, Liturujia Ibada ya Misa Takatifu na Sr. Tereza Awino na mada juu ya Malezi ya Watoto iliwasilishwa na Mariam Mlacha.

Aidha katika kilele cha kongamano hilo, kulikuwa na maandamano ya watoto yaliyokuwa na lengo la kusambaza mbegu ya uinjilishaji, kwanza kwa watoto wengine ambao bado hawajamfahamu Mungu bado lakini pia kwa watu wote. Ni katika maamdamano haya, kwa bahati nzuri baba Askofu Wolfgang Pisa OFM Cap wa jimbo la Lindi na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, aliweza kufanya maandamano pamoja na watoto na kwa namna ya pekee kuongoza misa katika kilele cha kongamano hilo.  Hakika, katika kongamano hili ni dhahiri kabisa kuwa watoto walisia mbegu ya uinjilishaji, kwao binafsi na kwa wengine waliokuwa nje ya kundi hili.

 

 

 

Imeandaliwa na: Pd. Paul Chembe, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa-Jimbo

Read more

KONGAMANO LA UTOTO MTAKATIFU JIMBONI SAME TAREHE 10-13/12/2024

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai na baraka nyingi alizotujalia mwaka huu.Tunamshukuru pia kufanikisha uwepo wetu katika kongamano letu la Utoto Mtakatifu. Tunamshukuru mlezi wetu mkuu yaani Baba Askofu kwa kutupa nafasi ya kukua katika malezi kwani “mtoto ni malezi” Mwaka huu tulifanikiwa kuleta nyumbani wazo la Kongamano la tano la Ekarestia kitaifa kwa kuwakutanisha Watoto wapatao 933 na walezi 76 jumla 1009 kwenye viwanja vya uaskofuni kwa muda wa siku nne.

Aidha, mada zilizowasilishwa kwa watoto ni pamoja na: Undugu huponya ulimwengu (Na Mwl. Silvano), Imani Katoliki (Na Mwl. Festo Hiza), Mtoto Mmisionari na uwajibikaji – Elimu, Wajibu na matokeo yake (Na Mwl. Silvano)Namna ya kuishi maisha ya furaha ukiwa Mtoto (Na Mwl. Festo Hiza), Haki ya Mtoto mmisionari kwa Kanisa na Taifa (Na Mwl. Silvano) Maisha ya Mtoto mmisionari kwa Watoto wenzake (Na Mwl. Festo Hiza),  Mashindano ya usomaji wa Biblia (Na Mwl. Silvano na Walezi Msista)

 

Walezi wa Utoto Mtakatifu walifundishwa ama kukumbushiwa juu ya Wajibu wa Mlezi katika Malezi (Na Mwl. Silvano)

MAFANIKIO

Watoto wamepata Malezi na mafundisho mblimbali kulingana na dhamira ya kongamano hususani Undugu unaoponya Ulimwengu na athari za kutokutambua haki za Mtoto. Walipata pia Sakramenti kama vile sakramenti ya Kitubio na Ekaresti Takatifu

MAPENDEKEZO YA WATOTO

  1. Watoto walipendekeza kuwa Walezi wawe na Kongamano lao wenyewe kutangulia kongamano la Watoto. Hii itawafanya kutoa malezi vizuri ikiwa wanajua wanachokifanya.
  2. Watoto walipendekeza kuwa Wazazi wasiwazuie Watoto wenzao kuja kongamano
  3. Watoto waliomba kuvumiliwa kwa usumbufu wao na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika malezi.

MWISHO

Siku ya kilele tulifanya Maandamano kabla ya adhimisho la Misa Takatifu ikiwa ni fursa kwa Watoto kuinjilisha kwa vitendo. Hakika tumeonja Uwepo wa Utukufu na Upendo wa Mungu kati ya Watoto na Walezi waliponywa na Yesu wa Ekaresti. Yote kwa Utukufu Wake.

 

Imeandaliwa na: Pd. Alphonce Ndaghine, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa – Jimbo  

                                            

Read more

KONGAMANO LA UTOTO MTAKATIFU JIMBO KATOLIKI LA NJOMBE – 2024

Kuanzia tarehe 26 Desemba 2024, Parokia mbalimbali za jimbo la Njombe; wamefanya makongamano ya Utoto Mtakatifu. Katika Parokia  ya Familia Takatifu-Utalingolo watoto walifundishwa mada zifuatazo: Haki na wajibu wa mtoto-iliyotolewa na Arodia Mkinga, Mtoto mmisionari-ilitolewa na Sr. Lucia Mpete OSB, Liturjia – Pd. Lucas Mgaya

Kulikuwa na mada zilizotolewa kwa walezi: Namna ya kuwafundisha watoto– Sr. Lucia Mpete OSB, Ulinzi na usalama wa mtoto-Arodia Mkinga

Dhamira kuu ya kongamano ilikuwa: Sisi Sote ni Wamisionari.

Jumla ya watoto washiriki katika Parokia mbalimbali ni 1,794 kadiri ya ripoti zilizotumwa katika Ofisi yetu ya PMS Jimbo. Katika kongamano hili, watoto walipata fursa ya kutembelea watoto walemavu na maskini na kuwapelekea zawadi ndogondogo.

 

 

Imeandaliwa na: Pd. Lukas Mgaya, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa-Jimbo

 

Read more

KONGAMANO LA UTOTO MTAKATIFU 26 – 29 DESEMBA 2024, MPANDA

Jimboni Mpanda, Kongamano la Utoto Mtakatifu mwaka huu limeanza tarehe 26 – 29 Desemba 2024. Tarehe 26 ilikuwa ni kwa ajili ya kuwasili. Tarehe 27 Des ilifanyika misa ya ufunguzi na bada ya hapo semina kwa watoto.

Watoto washiriki walikuwa 1,093, walezi 150, mapadre 12, masista 7 na Mha Baba Askofu na kufanyajumla kuu 1,263, ni sawa na ongezeko la asilimia 83 ya lengo kusudiwa.

Kwenye kongamano hilo, mada zilizotolewa ni mbili, ambazo ni;

  1. Unyanyasaji wa watoto – Pd Nicodemus Kyumana – Mkurugenzi wa PMS jimbo.
  2. Mazingira – Sr Mary Magdalene SND

 

Kilele cha kongamano kilikuwa tarehe 28 Desemba siku ya watoto mashahidi ambapo misa takatifu iliadhimishwa na Mha. Baba Askofu Eusebius Nzigilwa na kufuatiwa na chakuàla na burudani mbalimbali.

Tarehe 29 Desemba watoto walikuwa ni sehemu muhimu katika maadhimisho ya uzinduzi wa jubilei kuu kwa maandamano na misa takatifu iliyoadhimishwana Baba Askofu Eusebius Nzigilwa.

Baada ya Misa na chakula, na siku iliyofuata watoto walirudi maparokiani.

MAFANIKIO

  1. Ongezeko kubwa la ushiriki kwa watoto, walezi, mapadre na watawa.
  2. Ongezeko la ufahamu kwa watoto kutokana na mada wasilishwa.
  3. Ongezeko la hamasa la uundwaji wa kwaya za watoto.
  4. Ongezeko la ushiriki wa watoto wenye sare kwenye kongamano.

Tunamshukuru Mungu kwa ufanisi wa kongamano hili na tunatazamia maboresho na ufanisi mkubwa kwenye kongamano lijalo.

 

 

 

 

Imeandaliwa na: Pd. Nicodemus Kyumana, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa- Jimbo

Read more

TAARIFA YA KONGAMANO LA WATOTO JIMBO KATOLIKI LA MAFINGA

Tunamshukuru Mungu  kwa   zawadi  ya  uhai,  neema   na baraka  nyingi   atujaliazo  kila   siku  hadi tumehitimisha Kongamano  letu. Tunamshukuru pia kwa zawadi ya miaka 2025 ya Kuzaliwa Mwokozi wetu Yesu Kristo   ambaye ni zawadi ya Matumain i kwetu sisi wanadamu.

Washiriki

Kongamano letu limefanyika kwa siku   Tano na walikusanyika  watoto 902 na  walezi wao 74 kutoka Parokia zote za Jimbo Katoliki la Mafinga

Mada na Wakufunzi

Mada zilizowasilishwa ni kama ifuatavyo:  Wito –  Sr. Kil iana Sanga (CST), Mashirika ya Kipapa -Sr. Anagladness Mrumah (C.O.L.U, Fadhila – Pd. Gosbert Mlambia, Ulinzi na Usalama wa Watoto – Pd. Martin Mhavile, Yubilei Kuu 2025 – Pd. Paulo Wissa.

Mafanikio

Watoto walifanikiwa kupata mafundisho  juu   ya   Mashirika ya Kipapa,   Wito,  Fadhila Ulinzi na Usalama wa Mtoto na Dhamira ya Ybilei Kuu 2025. Pia watoto wamepata Sakramenti ya Kitubio na kuhimizwa juu ya majiundo kiroho na Kimaadili. Vilevile watoto walikula, walicheza, kuimba  na  kusali  pamoja  kwa  furaha.  Tukiongozwa  na  Baba  Askofu  wetu,  Vincent Cosmas Mwagala, tuliadhimisha 03/01/2025 Sherehe ya Watoto Mashahidi ikiwa ni Kilele cha Kongamano na Adhimisho la Yubilei Kuu 2025 Kijimbo  katika kundi la Watoto. Hakika tuliona uwepo wa Utukufu na Upendo wa Mungu kati ya watoto katika furaha yao ya kukusanyika Pamoja ndani ya Uzuri wa Mtoto Yesu. Furaha na Shangwe zilitanda Siku zote tano za Kongamano letu.

 

 

 

Imeandaliwa na: Pd. Gosbert Mlambia, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa- Jimbo

Read more

TAARIFA YA KONGAMANO LA WATOTO JIMBO KATOLIKI LA MBINGA

Kongamano la Utoto Mtakatifu jimbo la Mbinga, lilifanyika toka tarehe 27-29/12/2024 Uaskofuni Mbinga. Jumla ya watoto 1267 na walezi 91 walishiriki kongamano hilo. Watoto na walezi wao waliripoti tarehe 27/12/2024, na tarehe 28/12/2024 siku ya Jumamosi mada nne zilitolewa.

Mada ya kwanza ilikuwa EKARISTI TAKATIFU, iliyotolewa na Padre Erasto Nyimbo ambaye ndiye Mkurugenzi wa PMS Jimbo la Mbinga.

Ikafuata MADA YA ULINZI WA MTOTO, iliyotolewa na Padre Joseph Ngahy mkurugenzi wa Miito Jimbo la Mbinga.

Mada ya tatu ilikuwa ni MAADILI, ilitolewa na Padre Leander Ndimbo mwalimu na mlezi wa Seminari ndogo Likonde jimbo la Mbinga.

Mwisho mada ya MIITO MITAKATIFU, ambayo ilitolewa na Sr. Filotea wa shirika la Masista wa Mtakatifu Vincent wa Paulo Mbinga na mkurugenzi wa miito wa Shirika hilo. Kila mada ilitolewa kwa muda wa saa moja.

Tarehe 29/12/2024 Kongamano lilifungwa likitanguliwa na maandamano toka kanisa la hija la Mtakatifu Alois Gonzaga Mbinga mjini kuelekea Kanisa kuu. Watoto walitembea umbali wa kilometa mbili na robo, na wakati wote wa maandamano watoto waliimba nyimbo mbalimbali. Baada ya maandamano, iliadhimishwa misa ya kufunga kongamano la Utoto Mtakatifu na kufungua Jubilei ya mwaka Mtakatifu, misa ambayo iliongozwa na Mhashamu John Chrisostom Ndimbo, Askofu wa jimbo Katoliki la Mbinga.

 

 

Imetayarishwa na: Pd. Erasto Nyimbo, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa (PMS)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Read more

DIOCESE OF NJOMBE CHILDREN RECEIVING EDUCATION ON HOW TO RAISE FUNDS TO HELP THOSE IN NEED

During this Advent season, children of the Holy Childhood Society of the diocese of Njombe are in the process of receiving new education in every Parish on how to raise funds, aimed at helping people in difficult circumstances during the Christmas celebrations.

In line with this education that they are receiving from their leaders including the diocesan PMS Director Fr. Lucas Mgaya, they have decided to focus on praying the novena for Christmas which began on 16th December, while linking their prayers to the Almighty God so that their intentions may succeed.

 

 

From: PMS National Office

Read more

SAME CHILDREN HAD A CONGRESS, WITH A PREVIEW OF THE NATIONAL EUCHARIST OF THIS YEAR 2024

On 10-13 December 2024, children from the diocese of Same, had their Congress which has been held every year during the Advent period before 28th December. The theme of this Congress was that of the National Eucharistic Congress, which was held in September this year which says, “Fraternity to heal the world, we are all brothers”.

The topics presented at this Congress include: Sexual Violence, how to strengthen Spiritually, the role of the Virgin Mary as well as the meaning of pilgrimage considering that there are only a few days left to reach the holy year.

In fact, in this Congress children were very happy and they were even able to urge the Bishop not to get tired of organizing their Congress which will make them continue to strengthen spiritually and morally. However, with great maturity, they urged him to tolerate them as they recognized that they were property destroyers and miscreants, but while promising him to reform themselves so that they would not offend him when they arrived at his episcopate.

 

 

From: National PMS Office

Read more

CHILDREN FROM NACHINGWEA AND RUANGWA PARISHES VISIT EACH OTHER

In November 2024, children from the two Parishes of Nachingwea and Ruangwa from Lindi Diocese, visited each other in Nachingwa parish with the aim of praying, eating and playing together. In this small event, all the children from these parishes seemed to be very happy, as they were able to pray together with the aim of praying for their fellow children in these two areas who live in difficult circumstances, and on the other hand, praying for themselves so that they can find strength in their missionary work.

Also, the children had the opportunity to share their games from these two areas, which brought a great enthusiasm for wanting to continue living together in this place after each child made a friend or friends. After praying and playing, they sat and ate the food that had been prepared for them, and finally they dispersed to return home.

 

From: PMS National Office

Read more